Back to top

AFARIKI AKINYANG'ANYANA SILA NA MLINZI SHINYANGA

19 May 2022
Share

Jackson Joseph (55) mkazi wa kijiji cha Nyaligongo wilayani Shinyanga amefariki dunia wakati alipokuwa akinyang'anyana silaha na mlinzi wa kampuni binafsi ya Right Ndovu Security, baada ya walinzi wa kampuni hiyo kwenda kugombelezea ugomvi wa kifamilia wa Bwana Joseph ndipo mkasa huo ukajitokeza.

Kamanda wa polisi mkoani humo ACP.George Kyando amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.Ambapo wananchi wenye hasira kali ameenda kuvunja Ofisi ya kitongoji namba mbili ya Kijiji cha Nyaligongo na kuchoma moto Pikipiki ya Kamanda wa Sungusungu wakiwatuhumu viongozi hao kuhusika na tukio hilo la mauaji na kufumbia macho matukio ya unyanyaswaji kwa wananchi na wachimbaji ambayo yanaendelea katika kijiji hicho kwa muda mrefu.\

Wananchi wanaituhumu Sungusungu kuhusika na mauaji ya Bw.Joseph kwa wanachodai kwamba kufuatia ugomvi wa kifamilia wa Bw.Joseph, mkewe Joseph alienda kuripoti kwenye ofisi za Sungusungu ndipo wakachukua walinzi wa Kampuni binafsi kwenye kutanzua ugomvi huo wa kifamilia wa Bw.Joseph na Mkewe.