Back to top

AFARIKI KWA KUANGUKIWA NA JIWE, MTWARA

27 June 2023
Share

Said Hassan Nampali, mwenye umri wa miaka 60, Mkazi wa Kitongoji cha Mbulu, kilichopo wilayani Mtwara, mkoani Mtwara, amefariki baada ya kuangukiwa na jiwe, wakati akiendelea na shughuli zake za uchimbaji kokoto.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo, amesema tukio hilo limetokea jana, Juni 26, 2023, majira ya saa 9 alasiri, ambapo amewataka wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari wanapokuwa wanafanya shughuli zao.