Back to top

AFARIKI KWA KUNG'ATWA NA MJUSI WAKE.

23 February 2024
Share

Mwanaume mmoja wa Colorado Christopher Ward (34) amefariki baada ya kuumwa na mjusi mkubwa mwenye sumu 'Gila monster', ambaye alimfuga kinyume cha sheria kama mnyama wake kipenzi.

Ward alimiliki wanyama hao wawili wa kutambaa, na aliugua baada ya kung'atwa mkononi na mmoja wa wanyama hao.

Ward gafla alianza kuonyesha dalili za kutapika mara kadhaa, kabla ya kuzimia, na akawa hapumui tena.

Ward alipelekwa hospitali, ambapo aliwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua na baadaye alitangazwa kuwa ubongo wake amekufa.

Mijusi hao waliondolewa nyumbani kwa Ward wiki iliyopita na Crookston na maafisa kutoka Colorado Parks and Wildlife na Idara ya Maliasili.