Back to top

AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA TEMBO NAMTUMBO

18 February 2024
Share

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Milenia Lucas Magazini, mkazi wa Kijiji cha Likuyumandela kilichopo Kata ya Likuyuseka wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na tembo wakati akiwa shambani. 
.
Akizungumza na ITV Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Bi.Ngolo Malenya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza kuwa tembo aliyekuwa na mtoto alimuona mwanamke huyo kisha kuanza kumkimbiza na kumjeruhi, hali iliyosababisha kifo chake.
.
ITV imezungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo ambao wameitaka Serikali kuwapunguza wanyama hao kwani wamekuwa wakiwasababishia hasara kubwa ikiwemo kupoteza ndugu zao.