Back to top

Afisa Magereza feki, Geita atumia msamaha wa Rais kumtapeli kikongwe.

14 December 2019
Share

Kikongwe Bi.Ng'wasi Nine mkazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera ametapeliwa shilingi laki moja na nusu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Afisa Magereza mkoa wa Geita kwa lengo la kumsaidia mtoto wake apate msamaha wa rais kwa awamu ya pili hali iliyopelekea kikongwe huyo kulala kwa mwenyekiti wa serkali ya mtaa wa Katoma akiiomba serkali imsaidia kumkamata tapeli huyo.

ITV ilifika nyumbani kwa Mwenyekiti wa serkali ya Mtaa wa Katoma alipopewa hifadhi Kikongwe huyo aliyesafiri kutoka mkoani Kagera na kuja mkoani Geita akiwa na matumaini ya kumtoa mtoto wake gerezani.

Mwenyekiti wa serkali ya mtaa wa Katoma Evaristi Kaitana ambaye amempatia hifadhi kikongwe huyo  anasema amepewa taarifa za kutelekezwa kikongwe huyo na wasamaria wema baada ya matapeli hao kuchukua pesa hivyo akaamua kulifikisha jambo hilo kwa vyombo husika huku jeshi la polisi  likisema wameanza kuwasaka matapeli hao.

Akizungumza katika eneo hilo afisa mwandamizi wa TAKUKURU mkoa wa Geita Bahati Nzumbi anasema wameanza kuchunguza tukio hilo na ITV  ikamtafuta kwa njia ya simu mtuhumiwa anayeendesha utapeli huo kwa kutumia msamaha wa Rais.