Back to top

AGUNDUA MKEWE NI MWANAUME BAADA SIKU 12 YA NDOA YAO

30 May 2024
Share

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26, huko nchini Indonesia  amepatwa na mshtuko baada ya kugundua kuwa mkewe aliyefunga nae ndoa, siku 12 zilizopita hakuwa mwanamke bali alikuwa mwanaume aliyejifanya mwanamke kwa lengo kumlaghai ili ajipatie pesa.
.
Kulingana na mtandao wa South China Morning Post, umeeleza kuwa Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la AK, alikutana mwanaume huyo aliyejitambulisha kwa jina la Adinda Kanza (26), kwenye mtandao wa kijamii mwaka jana 2023, na walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya mtandao.
.
AK ameeleza kuwa tangu aanze kuwasiliana na Kanza kwa njia ya mtandao wakati wakiwa kwenye mahusiano, alikuwa akivaa mavazi ya kiislamu ambayo yalifunika uso wake wote, jambo ambalo ameeleza halikuwa shida kwake kwani aliamini binti huyo ana maadili ya kislamu na ni mcha Mungu.

Wawili hao baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja, walifanya mipango ya haraka ya kukutana ana kwa ana, na wakati wakipanga mipango ya harusi yao Kanza alidai kuwa familia yake haiwezi kuhudhuria harusi hiyo kwani hana wazazi.
.
Hata hivyo siku 12 baada ya harusi yao, AK, alianza kupata wasiwasi juu ya mkewe kwani alikataa kushiriki tendo la ndoa kwa madai kuwa yuko kwenye siku zake na alikuwa akikwepa kukaaa na kuzungumza na familia ya AK na alikuwa akivaa mavazi yake ya kujificha muda wote, hata akiwa na mumewe.
.
Baada ya wasiwasi huo AK alianza kumchunguza ndipo alipogundua kuwa Kanza ni mwanaume na alitambulika kwa jina la ESH, na wazazi wake wote walikuwa hai na wenye afya njema na walieleza kuwa hawana taarifa za mtoto wao kufunga ndoa.
.
Hata hivyo ESH alikamatwa na Polisi na alikiri kuwa amefanya hivyo ili ajipatie za AK na familia yake, ambapo mpaka sasa amezuiliwa na anakabiliwa na mashtaka ya ulaghai na anaweza kufungwa hadi miaka minne jela. via #SouthChinaMorningPost