Back to top

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mkewe

30 June 2020
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Katavi imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Bw.Susumo Shija (53) mkazi wa kijiji cha Mawiti Wilaya ya Mlele kwa kosa la kumuua mkewe aliyejulikana kwa jina la Ng'washi Nkuba kwa makusudi baada ya kumtuhumu kumuua mwanawe mdogo kwa imani za kishirikina
 
 
Akiendesha mashauri ya mauaji katika Mahakama hiyo, Jaji mMawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe.David Mrango amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 12, mwaka 2012 na kwamba mshitakiwa alikuwa na wake wawili
 
Aidha ameeleza kuwa mashahidi watano wa upande wa mashitaka akiwemo mtoto mkubwa wa mshitakiwa pamoja na balozi wa mtaa walithibisha na mshitakiwa kukiri mbele yao kuwa alimuua mkewe baada ya kuhisi amemuua kishirikina mtoto wa mke wake mdogo
 
Akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo wakili wa serikali Bwana Lugano Mwasubila amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa kumtuhumu kuwa mchawi.