Back to top

Ahukumiwa maisha jela mara mbili, kwa kulawiti.

23 September 2022
Share

Mwalimu wa Shule ya msingi Kyawazaru iliyopo wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Idrisa Athuman (29) amehukumiwa kifungo cha maisha, kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 14 na mwanafunzi wa darasa la sita huko wilayani Butiama .

Hii ni hukumu ya tatu kutolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma ikimuhusisha mwalimu huyo,ambapo hukumu ya kwanza alihukumiwa kufungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wake mara mbili,  na hukumu ya pili alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na sasa amehukumiwa tena kifungo cha maisha.