
Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini anayejulikana kwa jina la Sibongile Mani amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kufanyia matumizi makubwa pesa aliyoipokea kimakosa katika akaunti yake ya benki, ambapo mwanamke huyo alipokea Randi milioni 14 karibu $1m badala ya 1,400 alizostahili kupata huku akitumia karibu $70,000 katika maeneo 48 kote nchini hadi wakati akaunti yake ilipozuiwa.
.
Pesa hizo zilitoka kwa Mpango wa Kitaifa wa Msaada wa Kifedha kwa Wanafunzi (NSFAS) kupitia kampuni ya huduma za malipo, Intellimali, wakati mwanamke huyo alipokuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu, ambapo alitumia pesa hizo kununua nywele bandia, simu za rununu, pombe, godoro, kadi za zawadi na bidhaa zingine za kifahari.
