Back to top

Aishi juu ya Mti kwa siku 7 ashindia matunda na ndizi mbichi

08 February 2020
Share


George Mokoro mkazi wa kitongoji cha Genteme kijiji cha Buchanchari wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara ameeleza namna alivyoishi juu ya mti kwa muda wa siku saba ndani ya bonde la mto mara baada ya kuzingirwa na maji akiwa ameenda kuvuna mazao yake shambani ambayo pia yamesombwa na maji na kusalia bila chakula.

ITV ikiwa kijiji cha Buchanchari wilaya ya Serengeti mkoani hapa kufuatilia athari za mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zimepelekea kaya zaidi ya 400 kupoteza mazao na watu watano kufa ikapata taarifa za uwepo wa George Mokoro ambaye ameishi juu ya mti kwa muda wa siku nane baada ya kuzingirwa na maji akiwa shambani na mazao yake aliyokuwa akitegemea kwa chakula yakisombwa na mafuriko huku familia yake ikisalia bila chakula.

ITV ikafunga safari hadi nyumbani kwa baba huyo mwenye mke mmoja na watoto sita ili kujua nivipi amemudu kuishi porini juu ya mti na maswahibu aliyopata kabla ya kuokolewa na hali aliyonayo kwa sasa baada ya kupoteza chakula chote.

Mke wa Mokoro amedai anaujauzito wa miezi mitatu nakusema hali ya chakula nyumbani ni mbaya na kuiomba serikali uwasaidie.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kitongoji cha Genteme Petro Makori na baadhi ya majirani wemeeleza namna walivyopata taarifa na kumuoka mokoro na hali aliyonayo sasa  huku Mwenyekiti akieleza kuwa mbali na mokoro pia kuna wananchi wengine wanne bado wamezingirwa na maji.