Back to top

Aishi kwa maziwa na maji,baada ya kuanguka kwenye ngazi.

30 March 2020
Share

Mwanamke mmoja Maria Robhi (42)  mkazi wa kijiji cha Kwangwa a wilaya ya Musoma mkoa wa Mara amekuwa akiishi kwa kunywa robo lita ya maziwa na maji kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kuanguka kwenye ngazi za hospitali .

ITV imepata taarifa za mwanamke huyo kupitia wasamalia wema ndipo ikafunga safari hadi nyumbani kwake na kumshuhudia akiwa amalalala na hawezi kunyanyuka wala kutembea  na kudai ameishi maisha hayo kwa zaidi ya miaka kumi sasa huku akibubujikwa na machozi akiomba msaada.

NAMBA ZA KUMSAIDIA…0756866988

Mwanamke huyo ambaye anahitaji msaada alipata matatizo hayo  wakati akihangaikia matibabu ya watoto wake watatu ambao wanasumbuliwa na maradhi ya kifafa pamoja na mgongo wazi huku kijana wake mkubwa akiwa na hali mbaya zaidi kiasi cha kufungiwa ndani muda wote.