
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kuwa majeruhi wote wa ajali iliyohusisha magari manne katika eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha, wapewe matibabu bila kulipa gharama zozote.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt.Godwin Mollel, alipofika kuwajulia hali majeruhi 21 wa ajali hiyo, waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru, ambapo ameeleza kuwa majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndiye kapewa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC, Mkoani Moshi.
Akizungumza baada ya kusikiliza maelekezo hayo, mmoja wa majeruhi, Raia wa Togo, aliyejitambulisha kwa jina la Apelo Apeto (32), ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa huduma bora waliyompatia na anayoendelea kupatiwa hospitalini hapo.
.
"Kwa ajali hii ningekuwa nchini kwetu tayari ningekuwa nimepoteza maisha kwani kule bila kilipia huduma za matibabu hupatiwi huduma, lakini kwa Tanzania walivyowakarimu na weledi wameweza kuokoa maisha yangu mpaka sasa naendelea vizuri na naweza kuongea", ameeleza Apeto
.
Raia huyo amesema alikuja nchini Tanzania kwa semina ya mafunzo ya Uongozi iliyokuwa ikifanyika mkoani hapo na baadaye wakaenda kufanya utalii wa kuangalia kabila la wamasai wakati wanarudi ndo wakapata ajali hiyo.