Back to top

Ajali iliyo husisha Hiace na Toyota Land Cruiser yaua watu 6 Kahama.

22 July 2019
Share

Watu 6 wamefariki katika ajali ya basi dogo la abiria aina ya Hiace iliyogongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Land Cruiser katika barabara kuu itokayo Kahama kuelekea Kakola katika halmashauri ya Msalala usiku wa kuamkia leo.

Watu wanne walipoteza maisha hapo hapo na wawili wakafariki wakati wakitibiwa katika hospitali ya Kahama mjini. 

Kwa mujibu wa Frank Mshana ametueleza kuwa Jitihada za kumpata kamanda wa polisi zinaendelea licha ya Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Anamringi Macha kuthibitisha kwa njia ya simu baada ya kufika katika eneo la ajali.

Taarifa kamili kukujia endelea kutembelea mtandao wetu kwa taarifa zaidi.