Back to top

Ajali Shinyanga, Rais Samia atuma salamu za pole

09 August 2022
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Bi.Sophia Mjema, kufuatia vifo vya watu 16 , vilivyotokea katika ajali ya gari Agosti 08, 2022 , katika Kata ya Mwakata, wilayani Kahama.
.
Aidha Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali.