Back to top

Ajali ya Lori na Noah yauwa watano na kujeruhi wawili Dodoma.

03 July 2020
Share

KUTOKA DODOMA.

Watu 5 wamefariki 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la kibaigwa jijini Dodoma .

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha, huku akisema ajali hiyo imesababishwa na dereva wa Lori ambaye aliingia barabara kuu akitokea kituo cha mafuta bila kutoa tahadhari na ndipo ikatokea ajali.

Amesema hali ya majeruhi mmoja kati ya wawili ni mbaya sana hivyo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu, huku akibainisha kuwa dereva baada ya ajali alikimbia.

Kufahamu zaidi Bofya video hapa.