
Mlinda mlango wa Klabu ya MC El Bayadh ya nchini Algeria, Zakaria Bouziani, na kocha Msaidizi Khalid Muftah, wamepoteza maisha baada ya basi lililobeba timu hiyo, kupindika katika mji wa Sougueur, Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo.
Timu hiyo ilikuwa ikielekea Tizi Ouzou kumenyana na JSK Kabylie katika mchezo wa ligi uliopangwa kuchezwa siku ya Ijumaa.

Klabu hiyo imeandika kupitia mitandao yao ya kijamii kuwa wanachama wengine waliojeruhiwa wako katika hali nzuri.
Shirikisho la Soka nchini humo limeahirisha michezo yote iliyopangwa kufanyika wiki hii katika makundi yote.
