
Wanafunzi watano wa shule ya msingi Ndelenyuma katika halmashauri ya wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser la kampuni ya Kamsat.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa polisi Pili Mande amesema wanafunzi hao walikufa hapo hapo baada ya kugongwa na miili miwili ilikutwa barabarani huku miili mitatu ikikokotwa na maji hadi mita mia moja na kutupwa korongoni kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na mmoja akijeruhiwa.