Back to top

Ajichoma kisu kutokana na ugumu wa maisha

16 August 2022
Share

James Msengi mkazi wa Kota mkoani Tabora amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu kwenye koromeo akiwa katika kituo cha mabasi cha Msamvu, aliposhuka kununua muwa akiwa safarini kutokea Dar es Salaam kuelekea jijini Dodoma ambapo alipohojiwa amesema amefikia hatua hiyo kutokana na ugumu wa maisha.