Back to top

AJIFANYA MGANGA WA JADI KISHA KUIBA SIMU 5, DAR

20 February 2024
Share

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamtafuta mtu mmoja aliyejifanya Mganga wa jadi, katika maeneo ya Mji Mwema, Kigamboni, mkoani Dar es Salaam, kisha kuwanywesha dawa inayodhaniwa kuwa sumu na kuwalewesha watu 16 wa familia moja na baadae kuwaibia simu. 
.
Kulingana na Jeshi la Polisi mkoani humo, tukio hilo limetokea mnamo Februari 18, 2024, majira ya saa tatu usiku, wakati mtu huyo aliyejifanya Mganga, alipofika nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani, kwa lengo la kumtibia mke wake Bi.Fatuma Abdalla, aliyekuwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu, ambapo aliwanywesha dawa familia nzima, ambao walipoteza fahamu na akwaibia simu 5 za mkononi.
.
Jeshi hilo limesema wagonjwa wote walilazwa na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni na kwamba mpaka sasa 13 kati yao wameruhusiwa  na wengine watatu wanaendelea na matibabu.
.
Hata hivyo mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Jalala Ally Said, anashikiliwa na Jeshi hilo, akidaiwa kushirikiana na Mganga huyo.