Back to top

Ajifanya Shekh ili kutapeli fidia ya makaburi ya waislam Geita.

15 January 2021
Share

Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imeokoa shilingi milioni kumi na moja zilizotaka kutapeliwa na mtu mmoja  aliyejifanya  kuwa sheikh wa msikiti mkuu wa Geita kutaka kulipwa fidia ya makaburi ya waislam baada ya  halmashauri ya mji Geita kuchukua eneo la BAKWATA akidai kuwa yeye ni mmiliki wa makaburi yanayotakiwa kuhamishwa ili kupisha makazi na uwekezaji.
.
Kaimu kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita amewataka wananchi na taasisi za kidini kuwa makini na matapeli wanaojifanya viongozi wa dini na maofisa wa serkali kufanya vitendo vya kitapeli na kuwataka kutoa taarifa TAKUKURU ili wachukuliwe hatua.