Back to top

Al-Shabaab wauwa abiria 10 waliokuwa wakisubiri basi la usafiri Kenya.

06 December 2019
Share

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wamewauwa abiria 10 waliokuwa wakisubiri basi la usafiri wa umma la Madina lililokuwa likitoka hapa jijini Nairobi kuelekea Mandera.

Akithibitisha tukio hilo msemaji wa polisi Charles Owino amesema kuwa wanamgambo hao walivizia basi hilo na kulimiminia risasi katika eneo la kati ya Wargadadud na Kutulo.

Idadi kamili ya majeruhi bado haijulikani, Owino aidha amesema kuwa vikosi vya usalama vimetumwa eneo hilo kuwasaka washambuliaji.