Back to top

ALI BONGO KUWANIA MUHULA MWINGINE

10 July 2023
Share

Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba, ametangaza kwamba atawania muhula wa tatu, na kukaidi hofu za wapiga kura huku akizima uvumi wa kifo chake, kutokana na kuwa katika hali mbaya ya kiafya.

Bongo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alipatwa na kiharusi miaka mitano iliyopita, amekuwa akizungumziwa kuhusu afya yake, ikichochewa zaidi na kutoonekana kwake kwa umma, au katika shughuli zinazotangazwa moja kwa moja.

Lakini changamoto ya muhula wa tatu, imeweka mashaka kwa baadhi ya watu waliokaribu na rais huyo, aliyeingia madarakani mwaka 2009, akichukua madaraka kutoka kwa baba yake, Omar Bongo Ondimba, mtawala wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwa miaka 41