
Adam Kinyekile, mkazi wa Tunduma, mkoani Songwe, ambaye alibuni helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria wanne, lakini ikakosa kibali cha kuruka kwa sababu za kiusalama, ambaye kwa sasa amegeukia kwenye ubunifu wa mitambo na zana za kilimo, amepewa mkopo wa Tsh. Mil. 90/= na serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia, kwa ajili ya kununua vifaa kwenye karakana yake.

Akizungumza na ITV, Adam, ameishukuru serikali kumsaidia kutimiza ndoto zake ambapo amebainisha kuwa yupo kwenye hatua za awali za kubuni ndege isiyokuwa na rubani (Drone), itakayotumika kwenye shughuli za kilimo.

