Back to top

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM Afariki Dunia.

21 January 2021
Share

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Jachi Umbulla (Pichani hapo Juu) amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai Nchini India alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimetangazwa na Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai ambapo amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi itaendelea kutolewa.

Mhe.Job Ndugai amesema "Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe.Martha Umbullu, natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa Wabunge na wananchi wa mkoa wa Manyara, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu".