
Jeshi la Polisi nchini, limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyemuua Beatrice James Minja, kwa kumchoma kisu, mnamo Novemba 12, 2023, huko Tarakea wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.
.
Akitoa Taarifa hiyo, leo Disemba 31, 2023, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime, amesema Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake ni Lukas Paul Tarimo, alikamatwa akiwa amejificha katika Kijiji cha Jema, kilichopo Kata ya Olondonyosambu, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, na kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya kuua wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo na kumkimbiza katika kituo cha afya, ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri.
