Back to top

ALIYETUKANA VIONGOZI MTANDAONI ADAKWA, DAR ES SALAAM

01 August 2023
Share

Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema wanamshikilia Selemani Agai Gaya mwenye umri wa miaka 18, Mkazi wa Kigamboni, mkoani Dar es Salaam, akituhumiwa kuwatukana viongozi wakuu wa serikali nchini, kupitia mtandao wa Tik Tok.
.
Akitoa taarifa hiyo Muliro amesema kijana huyo alikamatwa mnamo Julai 29, 2023, na wanaendelea kumhoji, kwa ajili ya kumfikisha mahakamani, ambapo ametoa onyo kwa watu wote wanaotoa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria, limejipanga na kwamba litawafuatilia na kuwakamata.