
Mfanyabiashara Kaloli Mkusa (30) mkazi wa kijiji cha Msisina, mkoani Iringa, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na fidia ya Tsh. Milioni 1 na Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa kosa la kumbaka mama yake mzazi.
.
Hata hivyo, Mahakama hiyo imetoa hukumu bila tuhumiwa kuwepo mahakamani kwakua ametoweka na hajulikani alipo baada ya kuwekewa dhamana na baba yake aitwaye Joseph Mkusa ambapo tayari hati ya kukamatwa imetolewa na kwa mujibu wa Mahakama ataanza kutumikia kifungo hicho atakapokamatwa.
