Back to top

AMCHOMA MOTO MTOTO KISA KADOKOA NYAMA, GEITA

09 July 2023
Share

Kundi la wanawake wa Mtaa wa Ibobero, uliopo Kata ya Nyankumbu, mkoani Geita, wamevamia nyumbani kwa Bi.Anastazia Jackson na kumshushia kipigo, kwa madai kuwa amemchoma moto mdomoni pamoja na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili, mdogo wake mwenye umri wa miaka 2, akimtuhumu kudokoa nyama ya kuku iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni.
.
Wananchi hao wamedai kuwa tangu watoto hao watatu wafiwe na mama yao mzazi, Dada yao wa kambo, amekuwa akiwatesa, kwa kuwachoma moto, kuwanyima chakula na kuwatumikisha kazi ngumu.