
Herbert Kibukulia (50) mkazi wa Kijiji cha Okaulya nchini Uganda, anatuhumiwa kumchoma moto sehemu mbalimbali za mwili wake, Christopher Kalyebi (12) ambaye ni mtoto wake, anayesoma darasa la pili, akimtuhumu kunywa supu bila ridhaa yake.
.
Inaelezwa kuwa mtoto huyo alikunywa supu hiyo, baada ya kutoka shule akiwa hajala, hivyo alipoiona, akainywa ili apooze njaa, huku Baba yake akidai kuwa supu hiyo ilihifadhiwa kwa ajili ya chakula cha usiku.
.
Hata hivyo, Polisi kwenye eneo hilo wamesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo la kikatili alilofanyiwa mtoto huyo.
