Back to top

Amenusurika kifo baada ya kukwama ndani ya kontena tupu kwa siku 3.

13 May 2018
Share

Mtu mmoja  aliyetambuliakna kwa jina la Hassan  Haji Hassan amenusurika kifo baada ya kukwama ndani ya kontena tupu kwa siku tatu.

Akithibitisha tukio hilo kwasimu Kamanda wa polisi wa mjini Magahribi Hassan Nasser amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 36  amesema  siku ya Ijumaa akiwa anatoka kwenye kazi zake za uvuvi aliamua kupumzika kwenye eneo hilo  la kuhifadhia makontena  la malindi na usingizi ukamchuka na kujisahau,

Kamanda Nasser amesema eneo hilo ni la kila siku la kuhifadhia makontena yanayotoka bandarini na wahusika bila ya kujua walianza kuyahamisha makontena  hayo huku kijana  huyo akiwa  amelala  na kuweka juu ambapo alishindwa kujinasua na kubakia ndani ya kontena hilo kwa siku tatu.


Aliweza kuokolewa leo baada ya ya wafanyakazi wa bandari walipokuwa wakileta makontena mengine ndipo wakasikia kelele na za mtu kugonga na ndipo zoezi la uokoaji likafanyika na sasa kijana huyo amepelekwa hospitali na hali yake imerejea kama kawaida .

Wakazi wengi wa mjini wamekuwa na kauli tofauti huku wengine wakidai kijana huyo ni mtumiaji wa dawa za kulevya  na wengine wakadai alikuwa akitegemea kupakiwa katika meli za nje na aondoke nchini na wengine wakidai huyo kijana alikuja na kontena hilo kutoka nje madai ambayo kamanada nasser yote ameyakanusha.