
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema wanamshikilia Selemani Haruna (24), Mkazi wa Kimara Temboni, kwa tuhuma za kumuua Binti wa kazi za ndani, Editha Charles (22), na kuuficha mwili wake kwenye stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus.
.
Ambapo Kamanda huyo amebainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonesha Mtuhumiwa alifika kwenye nyumba aliyokuwa akiishi Binti huyo, akijifanya fundi umeme na kwamba alitakiwa kuweka Balbu ndipo alipomshambulia kwa kitu chenye ncha kali kisha akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba fedha kiasi cha Tsh 1,800,000/=.
