Back to top

AMUUWA MKEWE BAADA YA KUKATALIWA.

18 December 2023
Share

Polisi nchini Uganda wanamshikilia Dominic Babiiha mzee wa miaka 110 mkazi wa Kahunga, nchini Uganda, kwa tuhuma za kumchoma kisu mkewe mwenye umri wa miaka 109 hadi kufa kwa madai ya kumnyima unyumba.

Msemaji wa Jeshi la Polisi katika eneo hilo, Samson Kasasira amesema Wawili hao walienda kulala katika vyumba tofauti baada ya marehemu ambaye alikuwa hayuko sawa kiafya,  kukataa ombi la mume wake la kutaka kuambatana naye kitandani.

Tukio hilo limetokea siku ya kuamkia Jumamosi nyumbani kwao ambapo majirani wamesema walipofika walimkuta Bi.Costansio Bakasisa amefariki, huku mtuhumiwa akiwa amejifungia chumbani na amepoteza fahamu na pembeni yake akiwa na chupa ya kemikali ya kilimo.

Polisi walisema kwamba vurugu zilizosababisha kifo cha bibi huyo zilichochewa na “kumnyima mumewe haki yake ya ndoa,” na kwamba uchunguzi kuhusu suala hilo unaendelea.