
Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika,katika Kata ya Kashai,Manispaa ya Bukoba,mkoani Kagera amekutwa akichinja nyama ya mbwa kwa ajili ya kitoweo,, huku nyingine ikiwa imehifadhiwa na kutokufahamika wapi inapelekwa.
.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Vivianu Msigula, amewataka wananchi kuepuka kununua nyama ambazo hazijadhibitishwa na wataalamu ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuwakumba.
