Back to top

Anayejiita Mfalme Zumaridi akamatwa Mwanza

27 February 2022
Share

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Dianna Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi mkazi wa mtaa wa Buguku kwa tuhuma za kuhusika na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu zaidi ya 149 ambapo Jeshi hilo limebainisha kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akiwasafirisha watu hao toka sehem mbalimbali na kuwafungia nyumbani kwake ambapo alikuwa akiwatumikisha na kuwaaminisha kuwa yeye ni Mungu anayeponya, kufufua watu na kutatua matatizo yao.