Back to top

ANETI AHOFIWA KUFA AKIKAMATA SENENE MKOANI KAGERA

27 November 2023
Share

Aneti Kemilembe Godwin (14), Mkazi wa Kijiji cha Kibare, Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, anahofiwa kufa maji baada ya kutumbukia katika mto wa Kwambu ulipo Bukoba Vijijini wakati akikamata Senene.

Afisa Habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera, Sajenti Shabani Musa, akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Kagera amesema juhudi uokoaji zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi.

Aidha kwa mujibu wa Baba mzazi wa mtoto huyo, Bw.Godwin Anton, amesema tukio hilo limetokea wakati mtoto wake akiwa na mwezake wakitoka katika masomo ya maadalizi ya kijiunga na kidato cha kwanza mwakani.