Back to top

ANWANI ZA MAKAZI SASA MIEZI 5 BADALA YA MIAKA 5

19 January 2022
Share

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye amesema Serikali itatekeleza uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa muda wa miezi mitano badala ya miaka mitano kama ilivyokuwa itekelezwe hapo mwanzo.

Waziri Nape amesema zoezi hilo linafanyika kutokana na misingi mitatu ikiwemo Tanzania  ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta Duniani (UPU).

Mh Nape amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo hakuna mbadala isipokuwa ni kutekeleza kwa nguvu zote kwani Serikali inadhamiria kuwasaidia wananchi kuboresha mawasiliano katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi yao, sehemu zao za biashara na maeneo mengine ya huduma za kijamii.

Aidha, Waziri Nape amesema utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi ni jambo la kihistoria ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuacha alama kwa watanzania na lengo lake ni kurahisisha mawasiliano na kuifanya jamii kuwa ya kisasa zaidi bila kusahau kuimarisha ulinzi katika makazi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, bwana Abubakar Kunenge amesema zoezi la uwekeji wa anwani za makazi litarahisisha utambuzi wa maeneo ya shughuli mbalimbali za mkoa wa Pwani yakiwemo maeneo  ya viwanda.