Back to top

Apoteza maisha kwa kushambuliwa na tembo, Handeni.

30 April 2021
Share

Mtu wa pili amepoteza maisha ndani ya wiki moja baada ya kushambuliwa na tembo wanao endelea kuzurura hovyo kwenye makazi ya watu katika mtaa wa malezi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akiongea na ITV akiwa hospitali ya wilaya ya Handeni ulipohifadhiwa mwili wa marehemu ambaye amejulikana kwa jina la Mwanahawa Mohamed, mume wa marehemu amesema mke wake amekutwa na tukio hilo, asubuhi ya leo wakati akiwa na wajukuu zake wakichimba muhogo kwa ajili ya futari.
.
Aidha, Baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema kuwa hofu yao imeongezeka kutokana na tembo hawa kushindwa kudhibitiwa mpaka sasa hali inayo sababisha baadhi yao kushindwa kwenda mashambani kupalilia mazao yao huku waliopo mjini nao wakiwa hawana amani baada ya hivi majuzi tembo hao kupita karibu na makazi ya mkuu wa wilaya.