Back to top

ARDHI SACCOS ONGEZENI UBUNIFU KULETA MAENDELEO.

14 December 2023
Share

Katibu Mkuu wa Wizara  ya Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewahimiza wanachama wa Ardhi SACCO Ltd. kuongeza ubunifu zaidi ili kuleta hamasa ya maendeleo na kuwavutia wanachama wengi zaidi kujiunga na Chama hivyo.

Katibu Mkuu Mhandisi Sanga ameeleza hayo Jijini Dodoma leo wakati wa kufungua Mkutano wa Mwaka wa Ardhi SACCOS, Mkurugenzi wa Idara ya Milki Wizara hiyo Dkt. Upendo  Matotola akawataka wanachama hao kufanyakazi kwa bidii ili kufikia malengo ya SACCOS hiyo.

Kwa sasa Chama hicho kina 
wanachama 354 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo kulikuwa na wanachama 295 tangu SACCOS hiyo ianzishwe mwaka 2021 huku Wizara hiyo ikikadiriwa kuwa na watumishi takriban 2,300.

Aidha, Dkt. Matotola ameongeza kuwa, kila mwanachama anawajibu wa kuwa balozi na kuhamasisha watumishi wengine wa Wizara hiyo kujiunga na Chama hicho.

Akitoa taarifa ya Chama hicho Bw. Godfrey Machabe, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kuwa, malengo ya Ardhi SACCOS Ltd ni kuwawezesha watumishi wa Wizara hiyo kujikwamua kiuchumi katika maisha yao ya kila siku.