Back to top

ASILIMIA 25 YA WATU WANAKUFA KWA UGONJWA WA MOYO

27 March 2024
Share

Asilimia ishirini na tano ya vifo vya magonjwa ya moyo yanayoua watu wengi zaidi duniani, vinasababishwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dkt.Peter Kisenge, amesema hayo jijini Dar Es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Kisenge ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo amesema kwa kipindi cha miaka mitatu taasisi hiyo imewaona wagonjwa laki tatu, elfu sitini na moja, mia nane tisini na wanne wakiwemo watoto elfu thelathini, mia tatu thelathini na saba.

Amesema wagonjwa laki mbili, Elfu thelathini na nane, miana nane hamsini kati ya hao walikuwa na tatizo la shinikizo la juu la  damu.

Amesema asilimia tisini ya wagonjwa wa shinikizo la juu la damu hawana dalalili mpaka wapime wagonjwa na wachache miongoni mwao wanakuwa na dalili za maumivu ya kichwa, macho kuona kiza, maumivu ya misuli ya shingo, kutoka damu puani na wakati mwingine kupoteza fahamau, maumivu makali kifuani, kuzunguzungu, mapigo ya moyo kwenda kasi na kutoka damu puani.