Back to top

Asilimia 50 ya wanafunzi waliofaulu Arusha wadaiwa kukosa nafasi.

16 December 2018
Share

Ongezeko la wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mkoani Arusha limegeuka kuwa  janga kwa wazazi baada ya zaidi ya asilimia 50 ya waliofaulu kudaiwa kukosa nafasi ya kuanza masomo kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa.


Taarifa ya upungufu huo mkubwa wa vyumba vya madarasa imetolewa na Afisa elimu wa mkoa  huo Bw Gift Kiando katika kikao cha wadau wa elimu ambaye amesema hadi sasa kuna upungufu wa vyumba 374 ambavyo sio rahisi kupatikana kwa muda uliobaki.