Askari 11 wa jeshi la Israel wameuawa katika shambulio la kushtukiza la wapiganaji wa Wapalestina katika mji wa Khan Yunis, Kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Shirika la Utangazaji la Israel limesema jeshi la nchi hiyo linakabiliwa na hali ngumu katika Khan Yunis baada ya shambulio kubwa la kuvizia la wapiganaji wa Kipalestina.
Jeshi la Israel limesema litatoa maelezo kuhusu kile kilichotokea katika mji wa Khan Yunis.