Back to top

POLISI AFARIKI BAADA YA KUJERUHIWA MTWARA

03 February 2024
Share

Mkuu wa kitu cha Polisi Chiungutwa Wilaya la Masasi mkoani Mtwara, Inspekta Eliuterius Hyera, amefariki duania baada ya kujeruhiwa kwa bahati mbaya na askari mwenzake wakiwa katika harakati za kumkamata mtuhimiwa aliyevunja ofisi na kuiba.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo, ameseama siku ya tukio marehemu akiwa ameongozana na askari mwenzake katika ukamataji wa mtuhumiwa wa tukio la kuvunja ofisi na kuiba, ghafla mtuhumiwa huyo alianza kukimbia ili asikamatwe.

Amesema askari aliyekuwa na Bastola alifyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji, hivyo risasi hiyo ikapelekea kumjeruhi mkaguzi huyo na juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa hospitali ya Ndanda ambapo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.

Kamanda Katembo amesema juhudi za kuwasaka watu waliohusika katika tukio la wizi zinaendelea ili kuweza kuwafikisha mbele ya sheria.

Mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya ndanda kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anashikilia kwa hatua zaidi za Kisheria.

Aidha Hospitali ya Ndanda imekiri kutokea kiwa kifo cha askari huyo ambacho kimesababishwa na kuvuja damu nyingi sehemu ya kifua.