Back to top

Askari aliyemuokoa mtoto kwenye shimo la choo apandishwa cheo.

22 May 2020
Share

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga amempandisha cheo Danis Minja wa jeshi hilo kwa ujasili wake wa kuingia kwenye shimo la choo na kufanikiwa kumuokoa mtoto mwenye umri wa mwaka moja na nusu katika Kata ya Murgwanza wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Askari huyo wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji amepandishwa cheo kutoka Constable na kuwa Koplo.