Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Ruvuma yakiwekiwemo ya askari magereza wa gereza la Kitai wilayani Mbinga mkoani Ruvuma aitwaye Adam Kunwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani akiwa lindoni kwenye gereza la Kitai na askari wa jeshi la wananchi wa tanzania kumuua mwanajeshi mwenzake pamoja na raia kwa kuwapiga risasi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema kuwa mnamo disemba 27 majira ya jioni katika kambi ya jeshi la wananchi wa tanzania ya Chandarua wilayani Songea askari wa JWTZ Juma Mkele akiwa kazini pamoja na raia Veronika Kayombo waliuawa kwa kupigwa risasi na askari mwingine wa JWTZ aitwaye Batisin Samda akitumia bunduki aina ya SMG.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kusubiri uchunguzi wa daktari na kwamba upelelezi wa polisi unaendelea kuhusiana tukio hilo.
Katika tukio jingine kamanda Mushy amesema askari magereza aitwaye Adam Kunwa ambaye ni mganga katika zahanati ya ya gereza la Kitai akiwa lindoni alijiua kwa kujipiga risasi kichwani na kufariki na upelelezi wa polisi unaendelea.
Tukio jingine kamanda Mushy anabainisha kuwa mkazi wa kijiji cha Namahoka wilayani Namtumbo Bi. Zainabu Mohamed aligongwa na pikipiki wakati anavuka barabara na kupoteza maisha huku dereva wa piki piki iliyosabaisha ajali ambaye jina lake alikufahamika akitelekeza piki piki na kukimbia.
Wakati huo huo kamanda Mushy amesema jeshi la polisi limewafukuza kazi askari polisi wake watatu waliokuwa wakifanyia kazi wilayani Tunduru kwa makosa ya utovu wa nidhamu kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la hilo ambao ni Robert Elias Mkindo,Alex Sukuma Tenga na na Charles Anderson Magereja.