
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetakiwa kuweka kituo cha muda cha Askari wa Uhifadhi kitakacho hudumia vijiji vya Olchorapus, Imbibia na Engalaoni, wilayani Arumeru, kwa ajili kusaidia kulinda wananchi kutokana na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb), alipokuwa akijibu swali la Mhe. Noah Lemburis Saputu(Mb) aliyetakujua Serikali itajenga lini vituo vya Askari Wanyamapori katika Vijiji vya Olchorapus, Imbibia na Engalaoni wilayani Arumeru.
Aidha Mh. Kitandula alisema kuwa lengo ni kuwasogeza askari karibu na maeneo ya jamii kwa ajili ya kuwezesha udhibiti wa wanyamapori kwa wakati na kuepusha madhara kwa wananchi na mali zao.
