Back to top

ATCL yasitisha safari za nje kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona

24 March 2020
Share

Kampuni ya Ndege Tanzania itasitisha safari za nje za ndege zake kuanzia kesho Machi 25, 2020, hadi itakapotoa taarifa nyingine ya kuzirejesha safari hizo hali itakaporuhusu.

Taarifa ya kampuni hiyo imesema safari zitakazoathirika ni pamoja na Entebbe-Uganda, Bujumbura-Burundi,Hahaya-Comoro, Lusaka-Zambia pamoja na Harare-Zimbabwe.

Imesema kusitishwa kwa safari hizo kumetokana na mwendelezo wa matamko na maagizo yanayotolewa na serikali katika nchi ambazo ndege za kampuni zinafanya safari.

Imesema matamko hayo ni ya kufunga mipaka na kupunguza mwingiliano kwa sababu ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Taarifa hiyo imesema ndege za kampuni zitaendelea kutoa huduma katika safari za ndani japo kwa kupunguza miruko katika baadhi ya vituo kutokana na upungufu wa abiria wanaosafiri,hasa kipindi hiki ambacho tahadhari nyingi zinatolewa kwa umma kuachana na safari zisizo za lazima.