Back to top

Athari ya mvua Pembezoni mwa mto Msimbazi.

02 February 2020
Share

Nyumba zaidi ya kumi zimebomoka katika msimu huu wa mvua zilizopo pembezoni mwa mto Msimbazi maeneo ya Mabibo jijini Dar es salaam unaotanuka mwaka hadi mwaka.

Kufuatia tatizo hilo baadhi ya wananchi ambao nyumba  zao zimebomoka wamesema wamepata hasara kubwa kwani mto huo awali ulikiwa ni mfereji wa kuruka lakini kadiri siku zinavyo endelea mto huo hutanuka na kuleta madhara. 

Pia wananchi hao wamesema kuna baadhi ya nyumba zimeboka zote na nyingine zimeathirika  baadhi ya vyumba hatua iliyosababisha vyombo vya ndani kupelekwa na maji yakiwemo makabati makochi na TV .