Back to top

Athari za matumizi ya silaha kwa Mabavu Marekani kwa saa 24.

02 December 2019
Share

Idara ya Takwimu za Utumiaji Silaha kwa Mabavu Marekani imesema watu hamsini na wanne wameuawa au kujeruhiwa katika vitendo vya ufyatulianaji risasi nchini humo katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Vitendo hivyo vimeripotiwa katika majimbo ya Louisiana, Texas, Florida, na Washington DC.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi cha saa arobaini na nane zilizopita kumekuwa na vitendo mia moja hamsini na sita vya  ufyatulianaji risasi katika majimbo mbali mbali ya Marekani vilivyosababisha watu 52 kuuawa wengine  mia moja na wanane kujeruhiwa.