Back to top

ATHUMANI ADAIWA KUMUUA BIBI YAKE, MOROGORO

07 April 2024
Share

Athumani Mashaka (25), Mkazi wa Changarawe mkoani Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo, kwa tuhuma za kumuua Bibi yake aitwaye Agnes Karoli (70), mkazi wa Changarawe mkoani humo, kwa kumkata na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingo, baada ya kutokea mzozo kati yao.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, imeeleza kuwa linaendelea kukamilisha taratibu za uchunguzi ,ili mtuhumiwa achukuliwe  hatua za kisheria, ambapo pia limewataka wananchi kusimamia malezi kwa vijana ,ili kuepusha matukio kama hayo yanayoashiria mmomonyoko wa maadili.