
Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Wilbroad Ayebazbwe (34), mkazi wa Kamakanda wilayani Buhweju nchini Uganda, anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa bahati mbaya mtoto wake wa kiume wa miaka sita, wakati wakigombana na mkewe punde baada ya wawili hao kurejea kutoka Baa (Bar).
Taarifa za awali zinasema Wilbroad na mkewe Annet Ainembabazi (31), walikuwa wote Baa (Bar) na waliporudi nyumbani walianza kugombana ndipo baba huyo alipochukua panga kwa lengo la kumkata mkewe, lakini mkewe alikwepa na panga hilo likampata mtoto katika maeneo ya shingo.
Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mwanaume huyo aliyetoweka baada ya tukio, kwa tuhuma za mauaji na upelelezi ukikamilika atapelekwa mahakamani.Mke wa mwanaume huyo anasema mumewe amekuwa na tabia ya vurugu pale tu anapokunywa pombe.
